Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Wilson Charles Mahera

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Primary Question

MHE. DKT. WILSON C. MAHERA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza na kukamilisha utekelezaji wa ujenzi na ukarabati wa barabara katika Jimbo la Butiama?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. WILSON C. MAHERA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, wananchi wa Kata ya Kyanyari na Kata ya Masaba inayounganishwa na Jimbo la Bunda hawana barabara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imejenga daraja pale lakini wamekuwa wakisubiri kwa muda ili kuweza kupata barabara ili tuweze kuungana kati ya Bunda na Butiama. Vilevile ukija kwenye Kata ya Kyanyari unaungana na Musoma Vijijini pia hakuna muunganiko, kuna barabara inayokwenda Wanyere, daraja lina hali mbaya sana na limetengeneza bwawa. Kwa hiyo, ningependa kwa kweli katika bajeti hii fedha ziende ili kusudi barabara hizo mbili ziweze kupitika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili ni kwamba wananchi wa Kata ya Sirorisimba pamoja na Buswahili hawana muunganiko mzuri na wamekuwa wakisubiria barabara mpya mbayo inatakiwa kujengwa kati ya Kijiji cha Nyambili, inapita Nyandewa kwenda Buswahili. Ninaamini kwamba tumetenga kwenye bajeti lakini kutenga bajeti ni jambo moja na kupeleka fedha ni jambo lingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wamekuwa wanasubiri barabara hiyo kwa muda mrefu sana. Ninaomba kujua, je, barabara hiyo wakati huu itafunguliwa?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, nimpongeze sana Mheshimiwa Dkt. Wilson Charles Mahera, Mbunge wa Butiama, amekuwa Mbunge madhubuti na imara na anafuatilia sana ustawi wa wananchi wa Jimbo la Butiama. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Butiama kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, itaendelea kukupa ushirikiano kuhakikisha tunaboresha huduma za barabara katika Jimbo la Butiama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba ziko Kata ambazo hazijaunganishwa na kata nyingine katika Jimbo la Butiama na Serikali inaendelea kwa awamu kutenga fedha kwa ajili ya kufungua barabara nyingine, lakini pia kuziingiza kwenye mtandao unaohudumiwa na TARURA ili ziweze kupata bajeti kila mwaka kwa ajili ya matengenezo na ukarabati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge barabara hizo alizozitaja ambazo tayari alishawasilisha Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI. Tutaendelea kutenga fedha kwa awamu kuhakikisha kwamba zinatengenezwa, zinafunguliwa na zinaendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili tunafahamu kwamba katika barabara ambazo zimeathiriwa na mvua, mojawapo ni barabara katika Jimbo la Butiama. Tayari TARURA Mkoa wa Mara na Wilaya ya Butiama na Mheshimiwa Mbunge wameshaleta maombi ya shilingi bilioni 1,382 kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Buturi, Chuo cha Mwalimu Nyerere, Chifu Ihunyo, Kiwazaru, Kyatungwe, Mwibagi Store, Nyakiswa, Mang'atika, Rwamkoma, Kiabakari, Kamugegi, Mirwa na Sirorisimba. Maeneo hayo yote pamoja na hayo uliyoyataja tayari tuko kwenye hatua za kupeleka fedha kwa ajili ya kuanza ukarabati wa barabara hizo.

Name

Bakari Bakari Shingo

Sex

Male

Party

ACT

Constituent

Ukonga

Primary Question

MHE. DKT. WILSON C. MAHERA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza na kukamilisha utekelezaji wa ujenzi na ukarabati wa barabara katika Jimbo la Butiama?

Supplementary Question 2

MHE. BAKARI B. SHINGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa ninataka nifahamu kwamba Serikali ina mpango gani juu ya daraja la Kata ya Ukonga maeneo ya Saba Saba kuelekea Mongo la Ndege ambalo wakati wa mtangulizi wangu Mheshimiwa Jerry Serikali iliwahi kutembelea na ikaona umuhimu wa kulijenga tena daraja lile ambalo lilisombwa na maji?

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, nilitaka nilifahamu pia Serikali ina mpango gani...

MWENYEKITI: Swali la nyongeza ni moja.

MHE. BAKARI B. SHINGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inafahamu kwamba katika Jimbo la Ukonga tunalo daraja ambalo linahitajika katika eneo ambalo linaunganisha Ukonga kwenda Mongo la Ndege. Pia ni kweli kwamba Serikali ilishafika pale na kufanya tathmini na kuona gharama zinazohitajika kwa ajili ya ujenzi wa daraja lile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga kwamba Serikali bado ina mpango ule na dhamira ile. Kinachoendelea sasa ni utaratibu wa kibajeti ili mapema iwezekanavyo twende tukaanze ujenzi wa daraja lile baada ya kuweka vizuri masuala ya kibajeti.

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. WILSON C. MAHERA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza na kukamilisha utekelezaji wa ujenzi na ukarabati wa barabara katika Jimbo la Butiama?

Supplementary Question 3

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza. Barabara ya Msonza, Kimara inapita Magome, Ndengisivili mpaka Kimara, lakini barabara hii inaunganisha Kata tatu na barabara zake hazipitiki kabisa. Wananchi wanabebwa kwa machela kupelekwa kwenye vituo vya afya na hawana vituo vya afya. Je, lini Serikali itaona umuhimu ili barabara hii ijengwe, wananchi waweze kufika katika vituo vya afya salama?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, zipo barabara ambazo hazipitiki kutokana na athari ya mvua nyingi katika mwaka huu. Serikali imeshatoa maelekezo kwa Mameneja wa TARURA mikoa na wilaya kote nchini kwamba maeneo ambayo ni korofi na yanaathiri kupitika kabisa kwa barabara zile, ambayo ndani ya muda huu tunaweza kufanyia matengenezo pamoja na hali ya hewa ya mvua kuendelea, Mameneja watoe kipaumbele, wafike katika maeneo hayo wafanye tathmini na kufanya jambo linalowezekana kuwezesha wananchi waendelee kupita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, zile barabara ambazo zinawezekana kutengenezwa Serikali tutahakikisha tunafanya matengenezo ili wananchi waendelee kupita. Vilevile tutaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunatengeneza barabara hizo kwa ubora mkubwa zaidi. (Makofi)

Name

Khalid Mussa Nsekela

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyerwa

Primary Question

MHE. DKT. WILSON C. MAHERA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza na kukamilisha utekelezaji wa ujenzi na ukarabati wa barabara katika Jimbo la Butiama?

Supplementary Question 4

MHE. KHALID M. NSEKELA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru. Barabara ya Nkwenda, Kakanja, Kimuli hadi Mabira ni barabara kiungo kikubwa sana katika shughuli za uchumi kwa Jimbo la Kyerwa. Je, Serikali ina mpango gani wa kuikarabati na kuijenga ili shughuli hizo ziendelee?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, zipo barabara ambazo orodha yake tumeshazipokea kwa ajili ya ukarabati na ujenzi katika halmashauri mbalimbali, likiwemo Jimbo la Kyerwa. Pia zipo barabara ambazo tunaendelea kuzifanyia tathmini kwa ajili ya kuzifungua kwa maana ya barabara mpya kulingana na mahitaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, barabara hizo ambazo tayari zipo kwenye jimbo letu na zipo kwenye mtandao huo unaohudumiwa na TARURA, tutaendelea kuzitengea fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa Serikali inaendelea na tathmini za mwisho za athari ya mvua kwenye barabara hizo ili fedha ianze kutengwa na kupelekwa kwa awamu kwa ajili ya kufanya marekebisho; na tutahakikisha pia barabara hiyo ya Mheshimiwa Mbunge tunaipa kipaumbele.

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. DKT. WILSON C. MAHERA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza na kukamilisha utekelezaji wa ujenzi na ukarabati wa barabara katika Jimbo la Butiama?

Supplementary Question 5

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Sonu-Sawe kilomita sita, imekuwa barabara korofi sana, na kipindi hiki cha mvua haipitiki kabisa ilhali ndiyo barabara inayotumika kusafirisha mazao kama ndizi ambazo tunazitumia hapa Dodoma. Je, ni lini sasa Serikali itajenga barabara hii ili iweze kupitika?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, tulishakubaliana, na tumeweka mpango Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI kupitia TARURA kwamba kweli katika nchi yetu zipo barabara ambazo ni korofi mara nyingi. Kila mwaka msimu wa mvua zinakuwa korofi, zinaharibika kutokana na hali ya hewa na hali ya kijiografia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshakubaliana, kwanza, kuja na design ya aina ya barabara ambazo zitadumu zaidi katika maeneo yenye mvua nyingi, milima na hali za kijiografia ambazo zinaathirika kirahisi na mvua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, tunaendelea na utaratibu huo, na tutakapofika hatua ya kuwa na design ambayo tunaitekeleza, tutahakikisha barabara hiyo tunaiingiza kwenye design maalum ambayo itawezesha kukomesha kuharibika kila mwaka na kuitia hasara Serikali na wananchi. Kwa sasa tutaendelea kuifanyia matengenezo ya muda ili iendelee kupitika na kutoa huduma kwa wananchi wa Jimbo la Hai.

Name

Festo Richard Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Primary Question

MHE. DKT. WILSON C. MAHERA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza na kukamilisha utekelezaji wa ujenzi na ukarabati wa barabara katika Jimbo la Butiama?

Supplementary Question 6

MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi na Mheshimiwa Naibu Waziri tunapakana jimbo, na anafahamu kwamba majira haya mvua zimesimama. Kwa hiyo, wakandarasi wanatakiwa waingie site. Kwa Makete tuna barabara ya kutoka Ibaga kuelekea Mang’oto, Barabara ya Ukwama – Ihanga, Barabara ya Kinyika - Kikondo, na Barabara ya Ikuwo kule. Je, ni lini wakandarasi wataanza kujenga barabara hii, na hasa ukijua kwamba Serikali imeshatoa fedha na tayari wameshasaini makataba?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Mheshimiwa Festo Sanga ni jirani yangu, ninapakana naye katika Jimbo la Wanging’ombe. Ninafahamu kwamba anasimamia kwa karibu sana suala la barabara katika Jimbo la Makete, na Jimbo la Makete ni moja ya majimbo yenye mvua nyingi na hali yake ya kijiografia ni milima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekubaliana kwamba TARURA, Mkoa wa Njombe na Wilaya ya Makete, kwanza, tuendelee kuboresha aina ya barabara zinazojengwa, lakini pili, tuhakikishe kwamba wale wakandarasi wote ambao wamesaini mikataba na tayari wapo site, waendelee na kazi na kumaliza kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa wale ambao hawajaenda site, nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI kumwelekeza Meneja wa TARURA Mkoa wa Njombe na Meneja wa TARURA Wilaya ya Makete wafuatilie kwa haraka iwezekanavyo kuhakikisha kuwa wakandarasi wote wanakwenda site kwa ajili ya ujenzi wa barabara hizo kadiri ya mikataba na barabara zikamilike kwa wakati. Sisi tutafuatilia kuona utekelezaji wa barabara hizo.