Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 27 Water and Irrigation Wizara ya Maji 314 2026-05-12

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza: -

Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa mabwawa ya maji Mihingo, Tingirima, Salama, Lakana, Kambubu na Nyaburundu?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maji, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Boniphace Mwita Getere, Mbunge wa Jimbo la Bunda kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekamilisha ujenzi wa Bwawa la Mihingo lililopo Wilaya ya Bunda Mkoani Mara, ambapo lina uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 207.145. Aidha, katika mwaka wa fedha 2026/2027 Serikali itafanya mapitio ya usanifu wa kina kwa mobwawa ya Tingirima, Salama A, Lakana, Kambubu na Nyaburundu, ili kupata gharama halisi na kazi zitakazotekelezwa katika mabwao hayo, kwa kuwa usanifu wake umepitwa na wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya usanifu wa mabwawa hayo kukamilika, Serikali itatafuta fedha za kuanza utekelezaji wa mabwawa husika.