Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Boniphace Mwita Getere
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda
Primary Question
MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa mabwawa ya maji Mihingo, Tingirima, Salama, Lakana, Kambubu na Nyaburundu?
Supplementary Question 1
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaombe tu, wakati maswali yanapojibiwa hapa Bungeni, hatujibiwi sisi Wabunge, wanajibiwa wananchi. Kama hili suala la Mihingo kwamba anasema limekamilika, mimi ninamheshimu sana Mheshimiwa Waziri. Je, ni lini sasa ataenda Mihingo, mimi na yeye ili tukutane na wataalamu wake waliomwandikia mambo hayo ili tujue kwamba hili jambo limekamilika au bado?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Haya mabwawa yamekuwepo toka 2017/2018, na nilikaa na Wizara nzima Waziri akiwa Mbarawa, Bwira akiwepo. Wakatembelea jimbo zima kwenye vijiji 30 vya Tarafa ya Chamliho, wakasema mabwawa sita haya tutayachimba, upembuzi yakinifu ukafanyika. Je, ni lini sasa haya mabwawa yatachimbwa ili wananchi wale ambao walipisha maeneo yao ili waweze kupata maji?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa, na mimi ninampongeza kwa kazi nzuri anayoifanya na hasa kwa kufuatilia miradi inayotekelezwa ndani ya jimbo lake, na kwa kuendelea kuwasemea akina mama na kuendelea kuunga mkono falsafa ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo kichwani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni dhahiri kabisa kwamba Serikali ipo tayari kushirikiana na Mheshimiwa Mbunge kwenda jimboni kwake na kuhakikisha kwamba tunatembelea Bwawa hili la Mihingo. Mimi nitakuwa mtu wa kwanza kumpa ushirikiano kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji. Baada ya Bunge hili la bajeti niko tayari kwenda mpaka Bunda ili tukajionee.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, kama Mheshimiwa Mbunge alivyosema, haya mabwawa ambayo ameongelea feasibility study ilifanyika, detail design ikafanyika, ni mwaka 2016/2017. Kwa kawaida katika utekelezaji wa miradi ya maji, muda ukishapita, kuanzia miaka mitano, ni lazima tufanye mapitio ya ule usanifu ili tu-establish gharama halisi ili tuweze kwenda kutekeleza kulingana na mabadiliko ya ongezeko la watu na mabadiliko ya kifedha ya gharama ya manunuzi ya vitu ili tuhakikishe kwamba mradi huu tukishaanza kutekeleza tunaenda kuutekeleza katika uhalisia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tunamshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluh Hassan kwa sababu ya ununuzi wa mitambo ya kuchimbia mabwawa. Nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge, baada ya kufanya mapitio ya hii miradi ambayo iko katika jimbo lake, tutakwenda kutumia mitambo ambayo Mheshimiwa Rais aliinunua kwa ajili ya kuchimba mabwawa ili sasa ifikie mwisho wa huu mradi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninatambua kwamba umekuwa mradi wa muda mrefu, lakini nimtoe hofu kwamba sasa tunaenda kuhakikisha tunafikia mwisho katika hili.
Name
Mashimba Mashauri Ndaki
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Maswa Magharibi
Primary Question
MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa mabwawa ya maji Mihingo, Tingirima, Salama, Lakana, Kambubu na Nyaburundu?
Supplementary Question 2
MHE. MASHIMBA M. NDAKI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Ninawapongeza sana Wizara ya Maji kwa kutekeleza miradi mingi kwenye Jimbo la Maswa Magharibi. Tatizo ni moja tu, mkandarasi aliyejenga mradi wa maji Kata ya Zanzui, Kata ya Mwamashimba na anayejenga mradi wa maji Kata Malampaka hawajalipwa fedha zao. Ni lini fedha zao hawa wakandarasi watalipwa ili mkandarasi wa mradi wa Malampaka aweze kuendelea na kazi? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana na nimshukuru sana na kumpongeza sana kaka yangu Mheshimiwa Mashimba Mashauri Ndaki, Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi. Ni kweli kabisa tunayo madai mengi ya wakandarasi, lakini tunajaribu kupitia pia zile hati za madai na kujiridhisha na kazi ambayo imefanyika kule site. Baada ya kujiridhisha sasa Serikali inaandaa malipo kwa ajili ya kumlipa mkandarasi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge, hili tunaenda kulipa kipaumbele kuhakikisha kwamba mkandarasi huyu analipwa kwa haraka iwezekanavyo ili aweze kuendelea kuutekeleza mradi huu na ukatoe matokeo chanya ambayo yanatokana na sauti kubwa na ya kutosha ya mwakilishi wa Maswa Magharibi. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved