Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 27 | Energy and Minerals | Wizara ya Nishat | 315 | 2026-05-12 |
Name
Hasnain Gulamabbas Dewji
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilwa Kusini
Primary Question
MHE. HASNAIN G. DEWJI aliuliza:-
Je, mpaka sasa Visima Vingapi vya Gesi Asilia Vimechimbwa katika Kisiwa cha Songo Songo, na upi mpango wa kuongeza uzalishaji wa gesi?
Name
Salome Wycliffe Makamba
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Hasnain Gulamabbas Dewji, Mbunge wa Kilwa Kusini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kitalu cha Songo Songo kina jumla ya visima 12 ambapo Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) imechimba visima tisa na Kampuni binafsi ya Pan African Energy Tanzania imechimba visima vitatu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kitalu cha Songo Songo kinaendelea na uzalishaji wa gesi asilia ambapo kinazalisha wastani wa futi za ujazo milioni 84.7 kwa siku kulingana na uhitaji. Aidha, kutokana na leseni ya sasa kufikia ukomo mwezi Oktoba 2026, Timu ya Majadiliano ya Serikali (GNT) inafanya majadiliano na Mwekezaji Kampuni ya Pan African kuhusu uwezekano wa kuongeza kipindi cha pili cha leseni ya uendelezaji wa gesi asilia katika kitalu hiki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mara baada ya majadiliano kukamilika, TPDC na Pan African wataendelea na mpango wa uchorongaji wa visima zaidi. Ninaomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved