Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Hasnain Gulamabbas Dewji
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilwa Kusini
Primary Question
MHE. HASNAIN G. DEWJI aliuliza:- Je, mpaka sasa Visima Vingapi vya Gesi Asilia Vimechimbwa katika Kisiwa cha Songo Songo, na upi mpango wa kuongeza uzalishaji wa gesi?
Supplementary Question 1
MHE. HASNAIN G. DEWJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya kuongeza. Ninamuuliza Naibu Waziri, Songo Songo ilikuwa inapata mrabaha wa Serikali, lakini tangu 2019 mrabaha huo haujapatikana. Nimeongea na Halmashauri yangu ya Kilwa, mrabaha haujapatikana, na kijiji husika hakijapata 20% yake. Ninataka nijue, huu mrabaha utapatikana lini kwa Wilaya yetu ya Kilwa? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Songo Songo kuna adha kubwa ya maji. Ni kisiwa ambacho kina asili ya mwamba, hivyo kuna adha kubwa ya maji. Ninataka nijue, kwa kuwa uwekezaji mkubwa umefanyika Songo Songo, kwa adha hiyo, Serikali inasemaje kwa ajili ya wananchi wangu wanaopata shida sana ya maji? (Makofi)
Name
Salome Wycliffe Makamba
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Kwanza kabisa nimpongeze Mheshimiwa Mbunge, kwa kuwa na ufuatiliaji wa karibu wa namna ambavyo gesi asilia inaweza kuwanufaisha wananchi wa jimbo lake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Kilwa imekuwa ikinufaika na CSR, fedha ambazo zinatokana na uwajibikaji wa mwekezaji katika maeneo husika. Tumekuwa na makubaliano ya kulipa CSR na kwa miaka mitatu mfululizo, na tumeshalipa zaidi ya shilingi 900,000,000.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, kwa sababu ni haki yake kama mwakilishi wa wananchi kuweza kupata taarifa hizi, ninawaelekeza Wizarani waniletee kikokotoo cha malipo ya CSR ambazo zimefanyika hizo shilingi 900,000,000 katika eneo la Mheshimiwa Mbunge.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na kwenda kwenye kijiji, mara baada ya TPDC kupeleka kwenye halmashauri, halmashauri inao wajibu wa kugawa sasa fedha hizo kutokana na jinsi ambavyo watakubaliana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbunge ameuliza vizuri kuhusiana na kisima, ni kwa sababu TPDC kama sehemu ya CSR imechimba kisima cha maji. Tunafahamu pale kuna changamoto kubwa sana ya ile pampu kwamba ni ndogo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imetenga shilingi 400,000,000 kwa ajili ya kupeleka pampu mpya na tuweze kuzalisha maji zaidi ya lita 100,000. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, sisi kama Serikali, nia yetu ya dhati ni kuwatumikia wananchi na kuwafanya wanufaike na rasilimali zilizopo ndani ya nchi, na tutahakikisha kwa kufanya hivyo, tunawekeza kwenye miradi mbalimbali ya jamii kama sehemu ya kurudisha kwa wananchi kutokana na gesi ambayo tunaipata kwa ajili ya matumizi na kuendeleza uchumi wa nchi yetu. Ninaomba kuwasilisha.
Name
Najma Murtaza Giga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HASNAIN G. DEWJI aliuliza:- Je, mpaka sasa Visima Vingapi vya Gesi Asilia Vimechimbwa katika Kisiwa cha Songo Songo, na upi mpango wa kuongeza uzalishaji wa gesi?
Supplementary Question 2
MHE. NAJMA MURTAZA GIGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Mradi wa gesi asilia ni mradi mkubwa katika Taifa letu, na endapo utakamilika, utakuwa na manufaa makubwa kwa nchi yetu. Nini changamoto ya Serikali kwa mradi huu mpaka leo umeshindwa kukamilika na umekwamisha kazi hii ambayo ni ya muda mrefu?
MWENYEKITI: Majibu, Mheshimiwa Naibu Waziri. Mheshimiwa Najma Giga, tafadhali rudia swali lako.
MHE. NAJMA MURTAZA GIGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa gesi ni mradi mkubwa katika Taifa letu na umekuwa wa muda mrefu na ukikamilika utakuwa na manufaa makubwa kwa Taifa letu. Nini changamoto ya Serikali ambayo inakwamisha mradi huu usiweze kukamilika hadi leo?
Name
Salome Wycliffe Makamba
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze Mheshimiwa Najma Giga, amekuwa mshauri mzuri wa Wizara yetu ya Nishati kuhakikisha kwamba tunakamilisha mradi wa gesi asilia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, mradi huu umefika katika hatua ya mwisho kabisa. Pia, kama ulisikia wakati Mheshimiwa Waziri akihitimisha hoja yake wakati wa bajeti yetu ya Wizara ya Nishati, ameshakutana na wawekezaji kwenye mradi huu, wanamalizia hatua za mwisho za kisheria ili tuweze kwenda kuanza kuzalisha mradi huu. Ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge, sisi kama Wizara tunatamani sana kuona mradi huu unatokea kwa sababu tunajua ni mradi wa kimkakati ambao utaleta mapinduzi makubwa sana kwenye sekta ya gesi na maendeleo ya mikoa ya kusini.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved