Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 27 | Energy and Minerals | Wizara ya Nishat | 316 | 2026-05-12 |
Name
Abdallah Dadi Chikota
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nanyamba
Primary Question
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza: -
Je, lini usambazaji wa gesi asilia majumbani katika Jimbo la Nanyamba utaanza?
Name
Salome Wycliffe Makamba
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Abdallah Dadi Chikota, Mbunge wa Nanyamba, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya usambazaji wa gesi asilia nchini hususan katika Mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani na Dar es Salaam ambapo hadi kufikia Aprili, 2026 jumla ya nyumba 2,512 zimeunganishwa na miundombinu ya gesi asilia katika mikoa tajwa. Aidha, jumla ya nyumba 1,000 zimepangwa kuunganishwa kwa mwaka huu wa fedha 2026/2027.
Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa miradi hii ni endelevu, na unatarajiwa kufika sehemu mbalimbali nchini ikiwemo katika Jimbo la Nanyamba kwa Mheshimiwa Mbunge, kwa kuzingatia mahitaji, umbali kutoka ilipo miundombinu ya usafirishaji wa gesi asilia na upatikanaji wa fedha za kutekeleza miradi. Ninaomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved