Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 27 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 318 | 2026-05-12 |
Name
Jacquline Andrew Kainja
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JACQUELINE K. ANDREW aliuliza:-
Je, lini Serikali itaangalia upya gharama za uzalishaji wa Tumbaku ili Mkulima apate faida?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua kuwa gharama za uzalishaji wa zao la tumbaku zimekuwa changamoto kwa wakulima, hususan kutokana na kupanda kwa bei za pembejeo, gharama za nishati hasa kuni na makaa kwa ajili ya kukaushia tumbaku pamoja na riba za mikopo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Bodi ya Tumbaku na wadau imeanza kupitia mjengeko wa gharama za uzalishaji ili kuainisha maeneo ambayo yanaweza kupunguza gharama za uzalishaji ikiwemo pembejeo, tozo za vyama vya ushirika na mikopo ya benki. Aidha, Serikali imeanza vikao na benki zinazotoa mikopo kwenye zao la tumbaku kwa lengo la kujadili uwezekano wa kupunguza riba ya mikopo na gharama zinazohusu mikopo hiyo. Lengo ni kuhakikisha kuwa wakulima wa zao la tumbaku wanapata faida kupitia kilimo cha zao hilo.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved