Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 27 | Works, Transport and Communication | Wizara ya Ujenzi | 320 | 2026-05-12 |
Name
Thomas Maganga Kampala
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Katavi
Primary Question
MHE. THOMAS K. MAGANGA aliuliza: -
Je, lini ujenzi wa kiwango cha lami utaanza kwa barabara ya Inyonga – Majimoto hadi Kibaoni (km 162) kwa kuwa upembuzi yakinifu ulishakamilika?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Thomas Kampala Maganga, Mbunge wa Katavi, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeanza ujenzi wa barabara ya Kibaoni – Majimoto – Inyonga yenye urefu wa kilometa 152 kwa awamu ambapo mpaka sasa vipande vyenye urefu wa kilometa 9.3 vimekamilika katika center za vijiji vya Usevya kilomita 2.5, Majimoto kilomita 2.6 na Inyonga kilomita 4.2. Kwa sasa, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa barabara yote kwa kiwango cha lami.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved