Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Thomas Maganga Kampala
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Katavi
Primary Question
MHE. THOMAS K. MAGANGA aliuliza: - Je, lini ujenzi wa kiwango cha lami utaanza kwa barabara ya Inyonga – Majimoto hadi Kibaoni (km 162) kwa kuwa upembuzi yakinifu ulishakamilika?
Supplementary Question 1
MHE. THOMAS K. MAGANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza. Kwa kuwa barabara hii ni muhimu sana kwa wananchi wa Jimbo la Katavi, Kavuu na Mikoa ya Sumbawanga, Kanda ya Magharibi kwa jumla, je, Serikali haioni sasa kuna umuhimu wa kuweka fedha za kutosha ili hii barabara ikamilike kwa wakati na kuwaondolea usumbufu wananchi wa mikoa hiyo?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua sana umuhimu wa barabara hii, na ndiyo maana tayari tumeshakamilisha usanifu na tumeshaanza kujenga barabara kwenye ile miji mikubwa kwa kiwango cha lami. Pia ninamkumbusha Mheshimiwa Mbunge kwamba ndiyo maana tuna madaraja mawili ambayo tunajenga likwepo lile la Kavuu ili kuweza kuhakikisha kwamba tunapitisha malori makubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia wakati Mheshimiwa Waziri Mkuu amefanya ziara, alitoa maelekezo kwa Wizara kuhakikisha kwamba katika bajeti hii tunayoiendea, tuweze kuijenga hiyo barabara kwa kiwango cha lami, maelekezo ambayo Wizara inayafanyia kazi.
Name
Kijakazi Mohamed Yunus
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. THOMAS K. MAGANGA aliuliza: - Je, lini ujenzi wa kiwango cha lami utaanza kwa barabara ya Inyonga – Majimoto hadi Kibaoni (km 162) kwa kuwa upembuzi yakinifu ulishakamilika?
Supplementary Question 2
MHE. KIJAKAZI Y. MOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi kuweza kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa Barabara ya Mingoyo – Masasi kwa muda mrefu sana imekuwa mbovu na Serikali imeliona hilo, tayari mkataba umesainiwa, mkandarasi amepatikana na amepewa site kwa muda mrefu, lakini mpaka sasa kazi haijaanza. Ninaomba commitment ya Serikali, ni lini mkandarasi yule ataanza kazi na kukamilika kwake?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli barabara hii ya Mingoyo – Masasi imechakaa, lakini ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba tunavyoongea sasa hivi, ile barabara tunaifanyia ukarabati mkubwa ambao ni sawa na kuijenga upya kuanzia Mtwara – Mingoyo na Mingoyo – Masasi. Tumegawa katika lot mbili, kutoka Mtwara – Mingoyo na kutoka Mingoyo – Masasi kilometa 200 ambapo mkandarasi tulishampata, yupo kwenye maandalizi ya kuanza hiyo kazi tukisaidiana na wenzetu wa World Bank.
Name
Bonnah Ladislaus Kamoli
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Segerea
Primary Question
MHE. THOMAS K. MAGANGA aliuliza: - Je, lini ujenzi wa kiwango cha lami utaanza kwa barabara ya Inyonga – Majimoto hadi Kibaoni (km 162) kwa kuwa upembuzi yakinifu ulishakamilika?
Supplementary Question 3
MHE. BONNAH L. KAMOLI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuuliza, Serikali ina mpango gani na Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwa kuna barabara sasa hivi mbovu sana? Je, kuna mpango wa dharura ili barabara ziweze kutengenezwa? (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiachia mbali mipango ya Serikali ya kawaida, lakini pia tumeainisha barabara nyingi ambazo zimepata athari katika kipindi hiki ambacho mpaka sasa hivi mvua zinaendelea kunyesha, kuzikarabati kwa dharura tukiwa tunasubiri mpango wa kawaida wa kuzifanyia matengenezo makubwa barabara za Dar es Salaam.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tuna mpango mkubwa wa barabara nyingi ambazo tumeziweka katika mpango wa kuzijenga ili pia kupunguza foleni ikiwa ni pamoja na kujenga barabara nyingi kwa kiwango ambacho kinapitika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, zile ambazo tunahakikisha siyo lazima mtu apite kwenye barabara zile kubwa, basi hizi barabara ambazo zinakwenda zinaunganisha wananchi na wananchi ziweze kujengwa ili zitumike pia kama sehemu ya kupunguza msongamano mkubwa katika Mji wa Dar es Salaam.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved