Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 27 | Health and Social Welfare | Wizara ya Afya | 321 | 2026-05-12 |
Name
Mohamed Mussa Utaly
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lindi Mjini
Primary Question
MHE. MOHAMED M. UTALY aliuliza: -
Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi?
Name
Dr. Florence George Samizi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Muhambwe
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Afya, ninaomba kujibu maswali ya Mheshimiwa Mohamed Mussa Utaly, Mbunge wa Lindi Mjini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi unatekelezwa kwa awamu. Awamu ya kwanza na ya pili zimekamilika kwa gharama ya shilingi 4,000,000,000 ambapo sakafu ya kwanza imekamilika na inatoa huduma. Aidha, Wizara imeingia Mkataba kwa ajili ya ukamilishaji wa awamu ya tatu ambapo Mkandarasi ameanza kazi mwezi Novemba, 2025 kwa Mkataba wa miezi 12 na unatarajiwa kukamilika kabla au ifikapo mwezi Desemba, 2026.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mpaka sasa Mkandarasi ameshalipwa kiasi alichoomba jumla ya shilingi 812,000,000 kama hati ya malipo ya awali (Advance Payment). Aidha, Serikali itaendelea kusimamia ujenzi huo ili kuhakikisha unakamilika kama ilivyopangwa. Ninaomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved