Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 4 | Sitting 4 | Lands, Housing and Human Settlement Development | Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi | 42 | 2026-08-31 |
Name
Dickson Nathan Lutevele
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafinga Mjini
Primary Question
MHE. DICKSON N. LUTEVELE aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanzisha utaratibu wa kupima ardhi kwa bei nafuu kwa wananchi wa Kata za Isalavanu, Bumilayinga, Rungemba na Sao Hill?
Name
Kaspar Kaspar Mmuya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ruangwa
Answer
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Dickson Nathan Lutevele, Mbunge wa Mafinga Mjini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, gharama za upimaji ardhi kwa maeneo ambayo yameendelezwa hutozwa kwa kuzingatia Mwongozo wa Urasimishaji wa Mwaka 2021. Kwa mujibu wa mwongozo huo, gharama za kupanga na kupima kiwanja kimoja ni shilingi 130,000. Kabla ya hatua za Serikali kupunguza gharama hizi, wananchi walikuwa wanalipa kati ya shilingi 250,000 hadi shilingi 400,000, kwa ajili ya upangaji na upimaji wa kiwanja kimoja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa upimaji wa kawaida usiohusisha urasimishaji, gharama za upimaji zinatozwa kupitia Mwongozo wa Ukadiriaji wa Bei za Viwanja wa Mwaka 2016, ambao umeweka vigezo vya gharama za upimaji kwa kutegemea umbali eneo lilipo, ukubwa wa eneo linalopimwa, umbali kutoka alama za msingi, idadi ya vifaa vya kufanyia kazi na gharama za alama za mipaka (beacons) ambazo zinazohitajika. Ninaomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved