Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 4 Sitting 4 Natural Resources and Tourism Wizara ya Maliasili na Utalii 54 2026-08-31

Name

Mohamed Mussa Utaly

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lindi Mjini

Primary Question

MHE. MOHAMED M. UTALY aliuliza:-

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuendeleza vivutio vya utalii vilivyopo Lindi Mjini, ili kuongeza mapato na ajira kwa wananchi?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Mohamed Mussa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara inaendelea kusimamia na kutekeleza Sera ya Taifa ya Utalii ya Mwaka 1999, ambayo imetilia mkazo suala la kutanua wigo wa mazao ya utalii nchini kwa kubainisha vivutio na mazao ya utalii, kuyaweka katika mpango wa uendelezaji na utangazaji, ambapo katika mwaka wa fedha 2024/2025 lilifanyika zoezi la kubaini vivutio vya utalii katika mikoa 10 ikiwemo Lindi. Kwa upande wa Mkoa wa Lindi, mazao na vivutio vya utalii vilivyobainishwa ni pamoja na maeneo ya kihistoria, malikale, utamaduni na fukwe za bahari zenye fursa za kukuza utalii kupitia uwekezaji wa huduma na shughuli mbalimbali za utalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kutoka sekta za umma na binafsi, ikiwa ni pamoja na mamlaka zilizopo Lindi kuhakikisha vivutio vilivyopo mkoani humo vinaendelezwa. Aidha, Wizara kupitia Bodi ya Utalii Tanzania itaendelea kuimarisha mikakati ya kutangaza na kuvifikisha sokoni vivutio vya Lindi kwa kutumia majukwaa ya kidijitali, mitandao ya kijamii, maonesho ya utalii na kampeni mbalimbali za masoko ndani na nje ya nchi.