Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mohamed Mussa Utaly

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lindi Mjini

Primary Question

MHE. MOHAMED M. UTALY aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuendeleza vivutio vya utalii vilivyopo Lindi Mjini, ili kuongeza mapato na ajira kwa wananchi?

Supplementary Question 1

MHE. MOHAMED M. UTALY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamshukuru sana Naibu Waziri kwa majibu mazuri na ninaipongeza Serikali kwa kazi kubwa iliyoifanya ya kubainisha mazao ya utalii katika Mji wa Lindi. Maswali yangu ya nyongeza mawili ni haya yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Mheshimiwa Naibu Waziri haoni kuwa, kwa kitendo cha kubainisha vivutio hivyo vya utalii tangu mwaka wa fedha 2024/2025 na mwaka wa fedha uliofuata 2025/2026, kutofanyika chochote katika uendelezaji wa vivutio hivyo ni kuwanyima Vijana wa Lindi fursa ya ajira na kuikosesha Serikali mapato, ambayo yangeweza kupatikana kutokana na utalii katika vivutio hivyo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, je, katika mwaka huu wa fedha 2026/2027 ni vivutio vipi hasa vya utalii, katika Manispaa ya Lindi, vipo katika mpango huu wa kuendelezwa? (Makofi)

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mohamed Mussa, lakini kabla ya kujibu ninaomba nimpongeze sana kwa maswali yake mazuri yenye kujenga. Ninaomba uniruhusu nianze kujibu swali la pili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vivutio ambavyo vimebainishwa kule Mkoani Lindi ni pamoja na fukwe za Lindi Mjini, Kilwa, pamoja na sehemu za kihistoria. Maeneo ya kihistoria ya Vita vya Majimaji, kama kule Nandete pamoja na Tendaguru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la pili. Serikali imefanya jitihada mbalimbali baada ya kubaini vivutio hivyo, ikiwa ni pamoja na kuviweka kwenye mpango wa mwaka huu 2026/2027. Aidha, Wizara itaendelea kushirikiana na mamlaka mbalimbali za Serikali za Mitaa, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kule Lindi, pamoja na wadau wengine, ili kuendeleza vivutio hivyo kwa pamoja. Ahsante sana.