Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 4 Sitting 4 Youth, Disabled, Labor and Employment Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 46 2026-08-31

Name

Lucy Simirya Kombani

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. LUCY D. S. KOMBANI aliuliza:-

Je, hatua gani zinachukuliwa kuwalinda watoto dhidi ya ukatili mitandaoni kutokana na ongezeko la matumizi ya mitandao ya kijamii.?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kuchukua hatua za kuhakikisha watoto wananufaika na teknolojia huku wakilindwa dhidi ya ukatili, unyanyasaji, unyonyaji na madhara mengine ya kidijitali ambapo, miongoni mwa hatua hizo zinazotekelezwa ni kampeni ya kitaifa ya ulinzi na usalama wa mtoto mtandaoni, iliyofanyika katika Mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na iliyolenga kutoa elimu kwa wazazi, watoto, walezi na jamii kuhusu matumizi salama na yenye uwajibikaji na yanayolinda haki za watoto mtandaoni. Kupitia kampeni hiyo, zaidi ya watoto 1,811,212 wamefikiwa na elimu kuhusu usalama wa mtoto mtandaoni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Serikali imeunda Kamati ya Kitaifa ya Ushauri kuhusu Ulinzi na Usalama wa Mtoto Mtandaoni yenye jukumu la kutoa ushauri wa kitaalamu na kusaidia kuweka mikakati na afua madhubuti za kuzuia na kukabiliana na vitendo vya ukatili na madhara yanayoweza kuwakabili watoto wanapotumia mifumo ya kidijitali.