Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Lucy Simirya Kombani

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. LUCY D. S. KOMBANI aliuliza:- Je, hatua gani zinachukuliwa kuwalinda watoto dhidi ya ukatili mitandaoni kutokana na ongezeko la matumizi ya mitandao ya kijamii.?

Supplementary Question 1

MHE. LUCY D. S. KOMBANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Wizara na nitauliza maswali mawili ya nyongeza. Kumekuwa na matumizi makubwa sana nchini ya akili mnemba. Je, Wizara ina utaratibu upi wa kujiridhisha kwamba teknolojia hii haitokuwa kisababishi cha ukatili wa mitandaoni kwa watoto wetu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Kumekuwa na uingizwaji wa vifaa vya kielektroniki kama simu na tablet za watoto. Je, Wizara ina utaratibu upi wa kujihakikishia kwamba vifaa hivi havitaruhusu watoto hawa kupakua maudhui ambayo yatasababisha wao kupitia ukatili mtandaoni? (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote, ninapenda sana kumpongeza Mheshimiwa Lucy Kombani kwa ufuatiliaji wake wa karibu sana na kuona kwamba Kamati anayoifanyia kazi anaitendea haki, amekuwa akiuliza maswali mengi na ya msingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matumizi makubwa ya akili mnemba na teknolojia yasije yakasababisha madhara kwa watoto. Awali ya yote, ninapenda kusema kwanza maswali yake yote mawili moja kwa moja yanaingia kwenye Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Hivyo, ninapenda kusema nimeyapokea lakini sisi kama Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum tunafanya kazi na wizara nyingine ikiwemo Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye jibu langu la msingi hapa kwenye paragraph ya mwisho nimesema kamati ya kitaifa imeshaundwa na katika kamati hii tuna wajumbe wanaotoka kwenye Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Hivyo, masuala mazima ya matumizi makubwa ya akili mnemba tayari tunaendelea kuyajadili kuona namna njema kwa umoja wetu kudhibiti; tusikimbie teknolojia, dunia tuliyopo lazima watoto waishi ndani ya teknolojia na wanafahamu zaidi hata ya sisi wazazi. Kwa hiyo, hatuwezi kuwaondoa huko zaidi ya kuona kwamba kamati hii iende kufanya zaidi na kuhakikisha watoto wetu wanabaki salama huku wakiwa wazuri katika teknolojia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ninapenda kutoa wito wa malezi chanya kwa jamii, kila mzazi achukue jukumu la kuhakikisha anakuwa karibu na mtoto wake. Kifaa anachotumia mtoto wako umekinunua wewe, kama ni simu, kama ni tablet, umeinunua wewe, kwa hiyo pale unaponunua hakikisha programs ambazo mtoto anakwenda kuziangalia, kuzisoma, wewe mzazi uzifahamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haijalishi umri, hata akiwa zaidi ya miaka 18 mpaka miaka 25 hivi, tujitahidi kama wazazi na walezi, kuwaangalia kwa karibu, wakati mwingine kuwafanyia control. Unamvamia tu mtoto unamwambia hebu lete hiyo simu, fungua password, angalia anacheza na maeneo gani. Unaweza ukakuta wewe mwenyewe kiongozi mtoto wako huko mitandaoni anashiriki katika kujidhulumu yeye mwenyewe, anatuma picha mbaya ambazo kesho hata akipewa uteuzi wowote zinakwenda kumpa shida. Kwa hiyo, tuendelee kufanya malezi ya pamoja kuhakikisha kwamba teknolojia haitupeleki pabaya.