Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 4 | Sitting 4 | Justice and Constitutional Affairs | Wizara ya Katiba na Sheria | 48 | 2026-08-31 |
Name
Margaret Simwanza Sitta
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Urambo
Primary Question
MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza:-
Je, lini Serikali itajenga jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo Urambo kutokana na hali mbaya ya jengo lililopo sasa hasa kipindi cha mvua?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania imeendelea kutekeleza mpango wa ujenzi na ukarabati wa majengo ya Mahakama kwa lengo la kuimarisha miundombinu ya utoaji haki katika ngazi mbalimbali. Mpango huu unahusisha ujenzi wa majengo mapya na ukarabati wa majengo yaliyopo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa ujenzi wa jengo la Mahakama ya Mwanzo Urambo umepangwa kutekelezwa kwa bajeti ya mwaka 2027/2028.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved