Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Pauline Philipo Gekul
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Babati Mjini
Primary Question
MHE. PAULINE P. GEKUL K.n.y. MHE. SHANIF M. JAMAL aliuliza:- Je, lini Serikali itatoa fedha za ujenzi wa Barabara ya Magu – Ngudu – Hungumarwa kilometa 10 ambapo Mkataba ulishasainiwa?
Supplementary Question 1
MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Spika, niipongeze Serikali kwa kazi inayoendelea Kwimba; lakini nina maswali mawili ya nyongeza yanayotoka Babati.  Swali la kwanza; Mradi wa Bypass wa Babati ulipositishwa wakasema wananchi wale waliyoathirika Serikali itafikiria kuwalipa fidia na wananchi wameandika barua TANROADS.  Je, ni lini wananchi wale waliyoathirika na Mradi wa Bypass Babati Serikali itawalipa fidia? 
Mheshimiwa Spika, swali la pili; Barabara ya Babati – Kiteto – Simanjiro imechukua zaidi ya miaka 10 Serikali imekuwa ikijenga taratibu. Wananchi wa Manyara wamekuwa wakiathirika, wanapita Arusha na Kondoa.  Je, ni lini ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Singe – Kiteto – Simanjiro utakamilika? 
 
											Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
								NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kwa swali lake la kwanza, nitaomba Mheshimiwa Mbunge kama atapata nafasi niweze kulifanyia kazi kwa usahihi zaidi kuhusu fidia na hasa baada ya kuona Bypass ambayo ilikuwa imeainishwa. Kwa sasa tumesitisha ili niweze kujua kwenye fidia tumefikia hatua gani kuhusu madai ya wananchi wa Babati. 
Mheshimiwa Spika, kuhusu swali lake la pili linalohusu Barabara ya Babati kwenda Kiteto; tunajenga kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Hata hivyo, Serikali inaendelea kutafuta fedha ili tuweze kuijenga barabara hiyo yote kwa kiwango cha lami kwa sababu usanifu umeshakamilika. Ahsante. 
							
 
											Name
Timotheo Paul Mnzava
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Korogwe Vijijini
Primary Question
MHE. PAULINE P. GEKUL K.n.y. MHE. SHANIF M. JAMAL aliuliza:- Je, lini Serikali itatoa fedha za ujenzi wa Barabara ya Magu – Ngudu – Hungumarwa kilometa 10 ambapo Mkataba ulishasainiwa?
Supplementary Question 2
MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA: Mheshimiwa Spika, mvua zinazoendelea kunyesha kwenye maeneo ya Kaskazini, hasa Mkoa wa Tanga, zimeathiri sana miundombinu ya barabara na kukatisha mawasiliano kwenye baadhi ya maeneo. Je, Serikali ina kauli ipi juu ya hali hii? Ninakushukuru.
 
											Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
								NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ni kweli, mvua nyingi zinanyesha Mikoa ya Kaskazini, Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, Morogoro, Lindi pamoja na Rukwa; kuna mvua nyingi sana. Miundombinu kwa kweli imeathirika sana na hasa kwenye barabara ambazo ni za changarawe.
Mheshimiwa Spika, tunavyoongea sasa hivi tumeshaomba fedha kwa ajili ya fedha ya dharura ili kurejesha mawasiliano kabla ya kuanza kufanya matengenezo ya kawaida ambayo fedha tumeshatenga, lakini tuweze kupata fedha kwa ajili ya kuhakikisha kwamba mawasiliano yaliyokatika yanarejeshwa.  Ahsante.
							
 
											Name
Samweli Xaday Hhayuma
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Hanang'
Primary Question
MHE. PAULINE P. GEKUL K.n.y. MHE. SHANIF M. JAMAL aliuliza:- Je, lini Serikali itatoa fedha za ujenzi wa Barabara ya Magu – Ngudu – Hungumarwa kilometa 10 ambapo Mkataba ulishasainiwa?
Supplementary Question 3
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA: Mheshimiwa Spika, Barabara ya Mogitu – Haydom usanifu wa kina na upembuzi yakinifu umekamilika kwa bajeti ya Mwaka wa Fedha 2023/2024. Je, kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 barabara ile itafanyiwa kazi gani?
 
											Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba barabara tumekamilisha. Mheshimiwa Mbunge kama ataangalia kitabu tumeiweka kwenye mpango kwa mwaka ujao. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved