Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Dr. Christina Christopher Mnzava
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA K.n.y. MHE. ROSE V. BUSIGA aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha za kukamilisha ujenzi wa wodi ya mama na mtoto katika Kituo cha Afya Runzewe Mashariki – Bukombe?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nina maswali mawili ya nyongeza.  Swali la kwanza; kwa kuwa Halmashauri ya Mbongwe imetoa fedha za mapato ya ndani shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Nyakafuru (Jengo la OPD).  Je, ni lini Serikali itatoa fedha kwa ajili ya kukamilisha majengo katika Kituo hicho?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; je, ni lini Serikali itatenga fedha kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Nhomolwa Mbongwe?
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niipongeze Halmashauri ya Mbongwe kwa kutimiza wajibu wake wa kutenga fedha hiyo shilingi milioni 100 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Kituo cha Afya ambacho Mheshimiwa Mbunge Dkt. Christina, amekitaja.  Nimhakikishie kwamba Serikali kwa kutumia mapato ya ndani na kupitia fedha za Serikali Kuu, tutaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuhakikisha kwamba majengo yote katika Kituo hicho cha afya yanakamilika; na tutahakikisha kwamba kituo hicho kinaanza kutoa huduma mapema iwezekanavyo kwa masilahi ya wananchi katika eneo hilo.
Mheshimia Mwenyekiti, kwa swali la pili, kuhusiana na Kituo cha Afya ambacho tayari kimeorodheshwa kwenye idadi ya vituo vya afya vya kimkakati kwa kila jimbo; nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari Serikali inaendelea na taratibu za kutenga bajeti kwa ajili ya kwenda kujenga kituo hicho cha afya cha kimkakati katika kata ambayo Mheshimiwa Mbunge ameitaja.
							
 
											Name
Hassan Zidadu Kungu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduru Kaskazini
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA K.n.y. MHE. ROSE V. BUSIGA aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha za kukamilisha ujenzi wa wodi ya mama na mtoto katika Kituo cha Afya Runzewe Mashariki – Bukombe?
Supplementary Question 2
MHE. HASSAN Z. KUNGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata ya Namiungo kulikuwa kuna ahadi ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ya kujenga Kituo cha Afya katika Kata ile ya Namiungo. Vilevile, baada ya kuona mchakato ule ni mrefu sana na ahadi ile haikamilishwi, baada ya kuletewa fomu humu ndani za sisi Wabunge kujaza vituo vya kimkakati, nilijaza fomu ile kwa kuelekeza kituo kile kikajengwe Kata ya Namiungo ili kutekeleza ahadi ya Mheshimiwa Rais. Sasa ninataka kufahamu; je, ni lini pesa zile zitakwenda kwa ajili ya ujenzi wa Kituo kile cha Afya katika Kata ya Namiungo?
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Mheshimiwa Mbunge amefuatilia mara kadhaa kuhusiana na utekelezaji wa ujenzi wa Kituo cha Afya katika Kata ya Namiungo. Pia, tayari sisi kama Ofisi ya Rais, TAMISEMI, tulishakiweka kituo hicho kwenye Kata za Kimkakati na kwa bahati nzuri Mheshimiwa Mbunge mwenyewe alianisha kata hiyo kama kata ya kimkakati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tayari Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan amekwishatenga fedha shilingi bilioni 53.5 kwa ajili ya majimbo yote 214; na tayari hivi sasa fedha zimekwishaanza kupelekwa kwenye majimbo yote 120, jumla ya shilingi bilioni 30.  Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kituo hicho cha afya kitapata fedha wakati wowote mwaka huu, kwa sababu fedha zimeshaanza kupelekwa kwenye halmashauri zetu.
							
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved