Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Sebastian Simon Kapufi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpanda Mjini

Primary Question

MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI aliuliza:- Je, lini Taa za kuongozea Ndege zitafungwa katika Uwanja wa Ndege Mpanda?

Supplementary Question 1

MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru ninayo maswali mawili ya nyongeza. Kwanza, niishukuru Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utayari najua kwa maana ya Bandari ya Karema imejengwa kuna meli nne zinaendelea kujengwa kuna barabara ya lami inapelekwa Karema huo wote ni utayari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; Serikali inasema nini katika kufungamanisha Uwanja wa Ndege wa Mpanda na fursa nyingine zilizopo kama utalii na Soko la Kongo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; nini mkakati wa Serikali katika kusaidia Uwanja wa Ndege wa Mpanda kupata miruko iwe ni kutoka ATCL au makampuni mengine binafsi?

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru Mheshimiwa Kapufi, kwa maswali yake ya nyongeza mawili na nimpongeze kwa anavyofuatilia kwa karibu sana maendeleo ya mkoa wake na kipekee jimbo lake, lakini zaidi alivyotambua kazi kubwa ambayo Serikali imeshaanza kufanya katika eneo hilo la Mkoa wa Katavi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Serikali inatambua umuhimu mkubwa wa Mkoa wa Katavi pamoja na uwepo wa kuboresha ule Uwanja wa Ndege wa Mpanda na hii ni kutokana na ukweli kwamba, Katavi:

(i) Kuna utalii na sote ni mashahidi;

(ii) Madini ya kutosha;

(iii) Mazao ya kutosha;

(iv) Serikali inavyozungumza hivi inakamilisha ujenzi, maboresho ya reli ya kutoka Kaliuwa mpaka Mpanda na inaanza maandalizi mwaka wa fedha ujao 2025/2026 kujenga reli ya mita gauge kutoka pale Mpanda kwenda mpaka Kalema;

(v) Tayari tunajenga barabara ya lami kutoka pale Mpanda kwenda mpaka Karema; na

(vi) Tunajenga meli mbalimbali kwenye Ziwa Tanganyika yote haya na mengine ambayo sijayataja yanadhihirisha na kuthibitisha umuhimu wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Serikali tayari ninavyozungumza hapa imefanya makubwa katika Uwanja wa Mpanda. Kwanza, tumeshatengeneza na kukamilisha runway yenye urefu wa mita 2000. Pili, tayari tumejenga jengo la abiria la 1.4 bilioni na linatumika hivi navyoongea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwombe Mheshimiwa Kapufi akubali kwamba, jitihada hizi zinadhirisha na kuthibitisha dhamira ya dhati ya Daktari Samia Suluhu Hassan kuthamini na kutambua Mkoa wa Katavi. Hivyo basi, ninaomba nichukue jambo lake la taa za kuongozea ndege tuendelee kutazama huko mbeleni kadiri tukipata fedha tutaweza kujitahidi kuhakikisha kwamba, uwanja huu unakuwa na taa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, taa hizo pia kama nilivyosema kwenye swali la msingi zinategemeana sana na miruko, ninaomba nitumie nafasi hii kuzishauri na kuziomba kampuni mbalimbali za ndege nchini zilizo nchini na nje ya nchi kutazama fursa zilizopo katika Mkoa wa Katavi. Abiria wapo wa kutosha hebu tuongeze ndege, tukishaongeza ndege tutakuwa na miruko, tukiwa na miruko tuta-justify hata umuhimu wa kwenda kuweka taa za usiku kwa sababu ndege zitakuwa zipo za kutosha.

Name

Selemani Moshi Kakoso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tanganyika

Primary Question

MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI aliuliza:- Je, lini Taa za kuongozea Ndege zitafungwa katika Uwanja wa Ndege Mpanda?

Supplementary Question 2

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niipongeze Serikali kwa uwekezaji mkubwa sana uliowekezwa kwenye eneo la Mkoa wa Katavi hasa uwanja wa ndege pamoja na jengo la abiria na mengine ambayo Mheshimiwa Naibu Waziri ameyaeleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu ni kwambauuliza Serikali ilikuwa imeahidi kufanya miruko ya ndege kutoka Dar es Salaam, Mpanda hadi Lubumbashi. Ni lini Serikali itatekeleza ahadi ambayo ilikuwa imetoa?

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kumjibu Mheshimiwa Mwenyekiti wetu wa Kamati ya Miundombinu na Mbunge wa Kalema Mheshimiwa Kakoso kwamba, hoja yake tumeipokea na tunaendelea kuichakata Serikalini ili kutazama fursa zilizopo na uwezekano wa kuanza. Pia, Mheshimiwa Kakoso ninajua kuna suala ambalo amesahau kwa sababu tu pengine ni swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimjulishe pamoja na Wabunge wengine wa Mikoa mitatu Rukwa, Kigoma na Katavi kwamba, jana meli yetu ya MT-Sangara ilisimama kwa muda mrefu imeanza kufanya safari zake rasmi kutoka Kigoma kwenda Mpurungu kwenda Kalemii na kwenda Bujumbura. Hii ikiwa inamaanisha nini? Utekelezaji wa yale ambayo wanayaagiza Waheshimiwa Wabunge lakini Serikali ikiahidi.