Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Yustina Arcadius Rahhi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. YUSTINA A. RAHHI K.n.y. MHE. ZACHARIA P. ISSAAY aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Ofisi ya TRA katika Wilaya ya Mbulu?

Supplementary Question 1

MHE. YUSTINA A. RAHHI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, ni kweli TRA, Mbulu walikuwa na jengo la Ofisi limechakaa na lipo condemn, hawawezi kufanya kazi huko na ndiyo maana wanapanga katika ofisi ya halmashauri sasa kwa unyeti wa kazi za TRA, ni kwa nini Serikali isiharakishe kuwajengea ofisi?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, tunajua watoza ushuru wanaokusanya kodi hawapendwi sana mitaani. Kwa ajili ya utendaji mzuri wa kazi wa Maafisa TRA, Serikali ina mpango gani wa kuwajengea nyumba Maafisa TRA ikianza katika Mkoa wa Manyara? Ahsante. (Makofi)

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kabla ya kujibu maswali hayo ninaomba nimpongeze na kumshukuru sana Mheshimiwa Yustina Rahhi, maana yote hii inaonekana ni shauku ya maendeleo katika wilaya yake na hasa hasa katika suala zima la ukusanyaji wa mapato ya Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza, ni kweli kwamba jengo lililopo kwa sasa siyo rafiki, lakini Serikali imeona umuhimu wa ujenzi wa jengo hilo na ndiyo maana nasema mwaka unaokuja huo wa fedha 2025/2026 tutakwenda kujenga jengo hilo kwa ajili ya TRA.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili, tumepokea ushauri wake suala la nyumba kwa wafanyakazi wetu, tumelichukua na litaenda kufanyiwa kazi.