Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Atupele Fredy Mwakibete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busokelo

Primary Question

MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka gari la Polisi Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo?

Supplementary Question 1

MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze na kumshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kutimiza ahadi yake ya kutuletea gari la Polisi katika Jimbo la Busokelo.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kwamba tumepata gari moja la Polisi, lakini Jimbo la Busokelo ni kubwa na hivi ninavyoongea tuko katika ujenzi wa kituo kingine cha Polisi bonde la Mwakaleli. Je, ni lini Serikali itanunua gari lingine kwa ajili ya kuhudumia Bonde zima na kata zote zilizopo ndani ya Bonde la Mwakaleli? Ahsante sana.

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, katika jibu langu nimeeleza kwamba tayari tumepeleka magari mawili kwenye eneo hili la Busokelo. Kwa hiyo, uhakika ni kwamba tutawaongezea gari linguine. Ni mkakati unaoendelezwa na Serikali yetu ya Awamu ya Sita ambapo kwa sasa gari jipya linakwenda kuongeza nguvu katika lile gari la pili. Kwa hiyo, naomba awe na subira kidogo, kwani nchi ni kubwa kidogo hii, tunaendelea kusambaza na kwenye maeneo mengine.

Name

Condester Michael Sichalwe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Momba

Primary Question

MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka gari la Polisi Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo?

Supplementary Question 2

MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa nafasi. Jiografia ya Jimbo la Momba ni ngumu sana askari wetu kutekeleza majukumu yao. Je, ni lini Jeshi la Polisi litawasaidia askari wetu kuwapatia gari la Polisi liweze kufanya kazi kwenye Jimbo la Momba na siyo Jimbo la Tunduma?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, katika majibu ya juzi ambayo Mheshimiwa Naibu Waziri alitoa hapa Bungeni, alieleza mkakati wa Idara ya Polisi kununua magari na awamu ya kwanza ya mgao wa magari, tayari imeshaanza kusambazwa na bado kuna magari mengine yanatarajiwa kuingia nchini na hayo yatajali sana maombi ya Mheshimiwa Mbunge wa Momba kupatiwa usafiri.

Name

Dr. Charles Stephen Kimei

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vunjo

Primary Question

MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka gari la Polisi Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo?

Supplementary Question 3

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, Kituo cha Polisi cha Himo kinahudumia kata 16. Je, ni lini mtatupelekea gari kwenye kituo hicho? Ahsante sana.

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli tumpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia suala la huduma za Polisi katika maeneo ambayo yana uhitaji huo. Napenda tu kumwahidi, katika awamu inayofuata tutaangalia umuhimu wa Himo kupatiwa gari. Ahsante.