Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Selina Henry Kingalame

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SELINA H. KINGALAME aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuwaajiri wahitimu wahadhiri wa vitendo wanaojitolea sehemu za ofisi na vyuo hasa waliojitolea kwa zaidi ya mwaka?

Supplementary Question 1

MHE. SELINA H. KINGALAME: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipatia nafasi niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza na ninamshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri ya Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la kwanza, je, Serikali haioni haja ya kuwa na takwimu sahihi ya watu wanaojitolea katika taasisi na vyuoni?

Swali langu la pili; je Serikali ina mpango gani kwa ajili ya kutengeneza mfumo wa kuwatambua wahadhiri hawa wanaojitolea sehemu mbalimbali hasa vyuoni? Ahsante. (Makofi)

Name

Regina Ndege Qwaray

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa namna ambavyo ameendelea kuwasemea watumishi na wafanyakazi wa vyuo vikuu. Ninaomba sasa kujibu maswali yake mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ofisi ya Rais ya Utumishi wa Umma, imeendelea kuweka utaratibu mzuri na kuweka mwongozo. Hiyo ni hatua ya kwanza, kutoa mwongozo wa ajira ya kujitolea katika utumishi wa umma ili kwenda kuweka takwimu au kuwatambua wale watu wote ambao wanajitolea. Pia ofisi imeweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha kwamba kunakuwa na mifumo maalum itakayokusanya taarifa ya wale watu wote ambao wako katika mfumo wa ajira ya kujitolea.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii itatusaidia kwa kuwa tayari mwongozo umeshatoka, taasisi zote zitatumia mwongozo wa ajira ya kujitolea ili kuwatambua wale watumishi wote wanaojitolea katika utumishi wa umma.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukienda kwenye swali lake la pili, kama nilivyokwishaeleza kwenye swali la msingi kwamba ajira zote zitatolewa kwa ushindani ili kuweka haki na uwazi. Hivyo basi, Serikali imeendelea kusisitiza kwamba taasisi zote za umma zihakikishe zinatoa ajira kwa kuzingatia miongozo ya ajira ya kujitolea katika utumishi wa umma. Hata hivyo, Serikali imeendelea kuelekeza vyuo vikuu vya umma kuhakikisha kwamba vinatumia au vinaweka mfumo mzuri kwa wale vijana wote wenye uwezo au ufaulu mkubwa kuwatengenezea namna ya kuendelea kufundisha katika vyuo vikuu ili kuwajengea uwezo mkubwa kwa kuzingatia miongozo ya TCU na ajira ya kujitolea ya 2025, ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Christina Christopher Mnzava

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SELINA H. KINGALAME aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuwaajiri wahitimu wahadhiri wa vitendo wanaojitolea sehemu za ofisi na vyuo hasa waliojitolea kwa zaidi ya mwaka?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, kwa kuwa watumishi wetu, vijana wetu wanajitolea katika sekta ya afya pamoja na elimu wanapotuma maombi huwa wanaambatanisha ile barua ya taasisi ambayo walikuwa wanajitolea, kwa nini hawapewi kipaumbele?

Name

Regina Ndege Qwaray

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, kwanza ninampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa swali lake zuri la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyokwisha kueleza kwenye swali letu la msingi, kwa kuzingatia Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma kwamba ajira zote kwa sasa zinatolewa kwa njia ya ushindani ili kutenda haki kwa watu wote, ili kupata usawa, hivyo basi, msisitizo unaendelea kuwekwa kwamba vijana wanapopata nafasi ya kujitolea, wajitolee ili kujijengea uzoefu na wapate ujuzi na maarifa ili yale waliyoyapata darasani waende kuyatumia katika vitendo na mwisho linapotokea suala la ajira basi washiriki katika ushindani ili waweze kuajiriwa Serikalini.

Name

Esther Nicholas Matiko

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Tarime Mjini

Primary Question

MHE. SELINA H. KINGALAME aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuwaajiri wahitimu wahadhiri wa vitendo wanaojitolea sehemu za ofisi na vyuo hasa waliojitolea kwa zaidi ya mwaka?

Supplementary Question 3

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru na kwa niaba ya wananchi wa Babati Vvijijini pamoja na Tarime Mjini, maana mara kadhaa nimesikia ukilalamika pia, kuna watendaji na maafisa kilimo walioajiriwa kwenye idara ya afya na elimu wanajitolea sana lakini zikitolewa ajira hawapewi.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali haioni kwamba iweke hiki kigezo kama added advantage, wale wanaojitolea wapewe priority kama wanavyofanya wenzetu wa jeshini? Waliopitia jeshini wanapewa kipaumbele. Wale unakuta wamejitolea kwenye taasisi za umma wapewe kipaumbele inapokuwa imetangazwa ajira wanachukuliwa wao kwanza halafu ndiyo wanaenda kwa wale wengine?

Name

Regina Ndege Qwaray

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, ninapenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Esther Matiko.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama alivyosema kwamba watu wa Tarime pamoja na wa Babati Vijijini ambapo na mimi ni mdau mkubwa, ni ukweli usiyopingika wako vijana ambao tayari wanajitolea, lakini kwa kuona hivyo ndiyo maana nimesema Serikali imeweka utaratibu mzuri kuhakikisha wale vijana wanaojitolea wanaingia kwenye mfumo ni lazima kuwepo na ushindani.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunafanya hivi, tukubaliane na Mheshimiwa Mbunge kwamba ili kutenda haki kwa sababu siyo wote wanaopata nafasi ya kujitolea, lakini advantage ya yule anayejitolea, anapoenda kwenye ushindani tunaamini kwamba yule atafanya vizuri kwa sababu tayari ameishi katika maisha ya utendaji. (Makofi)

Name

Dr. Regina Christopher Malima

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SELINA H. KINGALAME aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuwaajiri wahitimu wahadhiri wa vitendo wanaojitolea sehemu za ofisi na vyuo hasa waliojitolea kwa zaidi ya mwaka?

Supplementary Question 4

MHE. DKT. REGINA C. MALIMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru sana kwa kunipa nafasi na mimi niulize swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri lakini swali langu dogo ni kwamba, wakati Serikali ikijipanga kuwa na mipango endelevu kwa ajili ya kuwasaidia wahitimu hawa wanaojitolea katika kufundisha vyuo vyetu, je, mna mpango gani wa haraka wa kuhakikisha mnawalipa posho na motisha wakati wakifanya kazi hii kwa uaminifu? Ahsante. (Makofi)

Name

Regina Ndege Qwaray

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Regina.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza Serikali kwa kuona kwamba inawezekana kuna watu wanajitolea katika taasisi nyingi, lakini katika shule zetu, katika vituo vya afya na wakati mwingine malipo au posho zile zinasuasua, Serikali imeleta mwongozo ambao unaeleza kiwango ambacho anatakiwa kulipwa na ndiyo maana katika mwongozo ule ambao umetolewa wa mwaka 2025 utaeleza utaratibu namna ya kuwapata wale vijana ambao wanakwenda kujitolea. Mwongozo unaeleza stahiki za yule mtumishi ambaye anakwenda kujitolea.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge nikutoe hofu kwamba utekelezaji wa mwongozo huu utatupeleka kwamba watumishi wote wanaojitolea watapata haki zao za msingi kila ambapo wanajitolea katika taasisi zetu lakini na katika maeneo yetu, ahsante.