Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Cecilia Daniel Paresso

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. CECILIA D. PARESSO K.n.y. MHE. ZACHARIA P. ISSAAY aliuliza:- Je, Serikali imefikia hatua gani katika kutekeleza Mradi wa Maji wa Kimkakati wa Tsoray katika Tarafa ya Nambis - Mbulu Mjini?

Supplementary Question 1

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa mradi huu unahitaji fedha nyingi ili uweze kutekelezwa, je, kwa nini Serikali isianze kutekeleza mradi huu kwa awamu ili kupunguza adha ya maji kwa wananchi katika maeneo husika?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, katika Kata ya Bara Wilayani Karatu kuna mradi wa maji uliokamilika na umejengwa na sekta binafsi ambapo takribani wananchi 15,000 wataenda kufaidika, je, Serikali ina mpango gani wa kuweka miundombinu ya usambazaji hadi kwenye vijiji vya jirani ili kupunguza kero ya maji katika vijiji husika?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Zacharia Paulo Issaay yaliyoulizwa na Mheshimiwa Cecilia Paresso, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi ni kweli kabisa fedha ni nyingi na nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa kutoa mawazo na ushauri wa namna ambavyo tunaweza kutekeleza mradi huu, na nikutoe hofu Mheshimiwa Mbunge tunapokea kwamba ni dhahiri kwamba inahitajika kuanza hatua kwa hatua ili tuone namna ambayo tunaweza tukafika. Hata hivyo, tutaangalia namna ambavyo tutaanza na chujio wakati tukiwa tunaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kujenga maeneo mengine ya kimiundombinu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, kwenye swali la pili kuhusiana na eneo la Karatu, Mheshimiwa Mbunge unafahamu mradi ule nilienda kuuzindua na kwa ushirikiano mkubwa sana na wadau wa maendeleo na wewe ukiwa sehemu ya kuhakikisha kwamba mradi ule unatoa matokeo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda nimtoe hofu chini ya Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, hakuna kijiji, hakuna mtaa, hakuna kata itakayobaki nyuma kwenye huduma ya maji safi na salama. Nikuhakikishie kwa kufanya hivyo tayari katika bajeti ya mwaka 2026/2027 tumeshaweka kiasi cha shilingi bilioni 1.6 kwa ajili ya kwenda kutengeneza mtandao wa kusambaza maji katika vijiji vya jirani ili waweze kupata huduma ya maji safi na salama.

Name

Festo Richard Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Primary Question

MHE. CECILIA D. PARESSO K.n.y. MHE. ZACHARIA P. ISSAAY aliuliza:- Je, Serikali imefikia hatua gani katika kutekeleza Mradi wa Maji wa Kimkakati wa Tsoray katika Tarafa ya Nambis - Mbulu Mjini?

Supplementary Question 2

MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri, Wilaya ya Makete imekumbwa na miradi chechefu ya maji, Mradi wa Maji Ipelele, Mradi wa Maji Usarimwani, Mradi wa Maji Kidope, Mradi wa Maji Magoe, Igofi, Uganga, Kisinga lakini Matamba. Miradi hii Serikali imelipa fedha, wakandarasi hawaonekani site na leo wamekuja viongozi wa chama, wa Serikali, wa chama hapa hapa Bungeni, wa kutoka Makete, Mwenyekiti na Katibu tunahitaji majibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lini Serikali mtaunda timu maalum iende Makete kufuatilia miradi hii ambayo imekwama kwa takribani miaka mitatu haijaendelea na majibu hayapo? Naomba majibu Mheshimiwa.

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Sanga kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, natambua hamu ya Mheshimiwa Mbunge na lengo la Serikali ni kupanga, kuanzisha miradi na kuikamilisha ili iweze kutoa matokeo. Hivyo basi kwa namna ambavyo Mheshimiwa Sanga ameliwasilisha, nitumie fursa hii kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji kumwelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Maji aunde hiyo timu mara moja iweze kufika Makete na kujiridhisha kwa nini mkandarasi alipwe na asiwepo site kwa sababu hizi ni fedha za walipa kodi wa Tanzania ambao wanatarajia kuona uwekezaji wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, unatoa matokeo chanya na wao waone ni sehemu ya Tanzania.

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. CECILIA D. PARESSO K.n.y. MHE. ZACHARIA P. ISSAAY aliuliza:- Je, Serikali imefikia hatua gani katika kutekeleza Mradi wa Maji wa Kimkakati wa Tsoray katika Tarafa ya Nambis - Mbulu Mjini?

Supplementary Question 3

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Wilaya ya Hai hasa mji wetu wa Bomang'ombe kipindi cha mwezi wa tisa kuelekea mwezi wa 12 kumekuwa na changamoto ya maji sana. Katika kutafuta ufumbuzi HUWASA Wilaya ya Hai kwa kushirikiana na bodi za maji zimefanya tathmini na kupata mahitaji ya shilingi bilioni 10 ili kuanzisha mradi mpya na chanzo kipya na kuondoa tatizo hilo. Nataka kufahamu kwa kuwa wameshawasilisha kwenye ngazi ya Wizara, Serikali ina mpango gani sasa mradi huu uweze kukamilika na tatizo la maji wilaya liweze kwisha?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Saasisha Mafuwe, Mbunge wa Hai na ninampongeze sana kwa kazi nzuri anayoifanya kwa Wana-Hai.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, ninamshukuru sana Mheshimiwa Mbunge kwa ushirikiano unaoendelea kutupatia kwa sababu hata hii CBWSO chanzo cha kuanza kuandika andiko tunatambua ulikuwa ni ushauri wako kwa kutumia window ya National Water Fund ambapo National Water Fund inatoa mikopo kwa taasisi zetu ili kuweza kutekeleza miradi ya maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda nimhakikishie kwamba andiko hilo limeshawasilishwa liko katika hatua nzuri kabisa za mchakato ili liweze kupelekwa Wizara ya Mipango na Uwekezaji kwa ajili ya idhini ili kuona kama andiko hilo ni viable katika uwekezaji wa huduma ya maji safi na salama. Lakini nikutoe hofu kipaombele cha Serikali ni kuhakikisha kwamba Watanzania wanapata huduma ya maji safi na salama.